Latest Posts

WAKILI AMBINDWILE AOMBA RIDHAA YA CCM IRINGA MJINI, AAHIDI MSAADA WA KISHERIA BURE NA ELIMU YA UCHUMI

Wakili Moses Ambindwile ni miongoni mwa wagombea sita walioteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania ubunge wa Jimbo la Iringa Mjini katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

Akiwa katika Kata ya Mivinjeni, Ambindwile aliomba kura za maoni kutoka kwa wajumbe wa CCM kwa lengo la kupata ridhaa ya chama kupeperusha bendera yake katika jimbo hilo lenye ushindani mkubwa wa kisiasa.

Ambindwile, ambaye ni mwanasheria kwa taaluma, alisema endapo atapewa ridhaa na hatimaye kuchaguliwa kuwa mbunge, atatoa kipaumbele katika utoaji wa msaada wa kisheria bila malipo kwa wakazi wa Iringa Mjini kupitia ofisi yake ya sheria.

“Najua changamoto nyingi zinazowakabili wananchi, hasa katika masuala ya sheria, mikataba, migogoro ya ardhi na familia. Nitajitolea kuwasaidia bila malipo,” alisema mbele ya wajumbe.

Mbali na hilo, Ambindwile ameahidi kutoa elimu ya uwekezaji, fedha na uchumi kwa wananchi, hasa wanawake, kwa lengo la kuwawezesha kuepuka mikopo kandamizi maarufu kama “kausha damu” ambayo imekuwa kikwazo kikubwa kwao kutokana na ukosefu wa elimu ya kifedha.

 

“Elimu ya kifedha ni muhimu kwa wananchi ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kifedha na kuondokana na utegemezi wa mikopo ya kinyonyaji ambayo imekuwa ikiwakandamiza hususan kina mama,” aliongeza.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!