Latest Posts

WALIMU WAKUU 8,851 NCHINI KUPATIWA MAFUNZO YA UONGOZI NA USIMAMIZI FANISI WA SHULE

Jumla ya walimu wakuu 8,851 watapatiwa mafunzo maalumu ya kuwajengea uwezo kuhusu uongozi na usimamizi fanisi wa shule yanayolenga kuimarisha uongozi na usimamizi wa shule wanazosimamia.

Mafunzo hayo yamefunguliwa Kitaifa rasmi tarehe 22 Septemba, 2024 jijini Mwanza na Mkurugenzi wa Uthibiti Ubora Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Bw. Ephraim Simbeye ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu, Prof. Carolyne Nombo aliyepata udhuru.

Akizungumza na walimu wakuu wa Mkoa wa Mwanza wanaoshiriki mafunzo hayo katika hafla ya uzinduzi wa mafunzo hayo Bw. Simbeye amewataka walimu wakuu wanaoshiriki mafunzo kuhakikisha wanazingatia yote watakayofundishwa na kwenda kuyatekeleza kwa vitenzo hasa katika maeneo ya usimamizi wa ujenzi wa miundo mbinu, utunzaji wa kumbulumbu, usimamizi wa ufundishaji na ujifunzaji na utunzaji wa takwimu za elimu shuleni.

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu ikiwa ni katika awamu ya tatu ya mafunzo hayo ikihusisha jumla ya walimu wakuu 8,851 katika Mikoa 13 ya Tanzania Bara. Awali mafunzo hayo yaliendeshwa katika awamu ya kwanza ikihusisha walimu wakuu 4,522 katika Mikoa 7 na awamu ya pili ilihusisha walimu wakuu 4,620 katika Mikoa 6 ya Tanzania Bara na yametekelezwa chini ya mradi wa BOOST.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!