News, Njombe.
Mamia ya wafuasi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wakazi wa mkoa wa Njombe wasio na upande wa kisiasa wameshiriki maandamano ya amani yaliyofanywa na chama hicho kuunga mkono maamuzi ya wajumbe wa mkutano mkuu taifa kwa kitendo cha kumpitisha Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea pekee wa chama hicho kwenye nafasi ya Urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwa mwaka huu.
Katika uteuzi huo uliofanyika katika kikao cha Januari 18-19 mkoani Dodoma, CCM pia ilipitisha jina la mgombea mwenza kwa nafasi ya makamu wa Rais anayechukua nafasi ya Dkt. Philip Mpango ambapo kwa kauli moja walikubaliana kumpitisha Dkt. Emmanuel Nchimbi ambaye kwa sasa anahudumu kwa nafasi ya Katibu Mkuu wa chama hicho.
Katibu wa Siasa na Uenezi mkoa wa Njombe, Josaya Luoga katika maandamano hayo ya pongezi na mapokezi amesema mkoa wa Njombe unasimama na mama kwa kazi nzuri aliyofanya kwa kipindi chote alichotumia kwa nafasi ya Rais wa Taifa hili.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Njombe Dkt. Scholastika Kevela wanaunga mkono maamuzi ya mkutano mkuu taifa kwasabu zipo sababu
“Tunazosababu za kuwapitisha kwa kishindo na sisi watu wa Njombe kuunga mkono na kubwa ni kutokana na utekelezaji mzuri wa Ilani”