Latest Posts

WANAFUNZI WA SEKONDARI KUANZA MASOMO YA UFUNDI STADI.

Na Josea Sinkala, Mbeya.

Serikali wilayani Mbeya mkoani Mbeya imewataka wazazi na walezi kupokea maboresho ya mtaala wa elimu ya msingi na sekondari ili kuendana na mabadiliko ya Dunia ya sasa kwa watoto kusoma masomo waliyo na uwezo nayo kwa faida yao baada ya kuhitimu elimu ya sekondari.

Akizungumza na Jambo TV wilayani Mbeya baada ya mafunzo mafupi kwa maafisa elimu kata na wakuu wa shule za sekondari katika Halmashauri ya wilaya ya Mbeya, afisa mthibiti ubora wa shule wilaya ya Mbeya Mary Makali, ameipongeza Serikali kupitia wizara ya elimu kwa uboreshaji sekta hiyo.

Amesema lengo la Serikali ni kuboresha sekta ya elimu ikiwemo kujengwa shule za amali kila mkoa na kuweka miundombinu rafiki kwenye shule za sekondari ili watoto kujifunza masomo ya sekondari na ufundi stadi ili kupata ujuzi wakiwa shuleni badala ya kusubiri wahitimu na kutarajia kwenda kuajiriwa pekee.

Amesema maboresho hayo yameingizwa kwenye mtaala wa elimu na utazinduliwa rasmi na Mhe. Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan mwishoni mwa mwezi huu (Januari 2025).

Kwa upande wake Moses Mulungu kutoka ofisini ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya, amewaasa maafisa elimu sekondari na wakuu wa shule wilayani humo kwenda kufikisha elimu hiyo kwa jamii na wanafunzi ili kuendana na maboresho ya mtaala huo wa elimu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!