Latest Posts

WANAJAMII WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUTUNZA RASILIMALI ZA MAJI

Meneja wa Mazingira na Usimamizi wa Jumuiya ya Watumia Maji ambaye pia ni Afisa Maendeleo kutoka Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, Janeth Kisoma ameitaka jamii na makundi yote kushirikiana kwa pamoja kutunza rasilimali za maji kwaajili ya kizazi cha sasa na baadaye.

Kisoma amezungumza hayo mkoani Morogoro katika wiki ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani wakati jumuiya hiyo ilipotembelea Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira ambapo amesisitiza kuwa ni wakati sasa wa jamii kushirikishwa katika utunzaji wa rasilimali za maji.

Ameongeza kwa kusema katika wiki ya maadhimisho ya siku ya wanawake, wanawake Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu wameamua kushirikiana na jamii katika kupanda miti katika Shule ya Msingi Mwere iliyopo Manispaa ya Morogoro, kutembelea wodi ya wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro pamoja na kuwatembelea wafungwa katika Gereza Kuu la Wanawake Kingolwira huku elimu ya utunzaji wa mazingira na rasilimali za maji ikitolewa

“Sisi wanawake wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu leo tumepanda miti katika shule ya msingi Mwere, tumewatembelea wanawake wenzetu hospitali na gerezani lengo likiwa ni kuwatia moyo na kuwafariji, na kikubwa kutoa elimu ya umuhimu wa kutunza rasilimali za maji”, ameeleza Kisoma.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!