Latest Posts

WANANCHI CHATO WANUFAIKA NA MITAMBO MPYA YA KUKARABATI BARABARA

Mbunge wa Jimbo la Chato Kusini, Paschal Lutandula, amekabidhi mitambo ya kisasa ya kukarabati barabara yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja kwa ajili ya kuboresha miundombinu katika mitaa, vijiji na kata za jimbo hilo, hatua inayolenga kurahisisha usafirishaji wa mazao na kuimarisha shughuli za kiuchumi kwa wananchi.

Hafla ya makabidhiano hayo imefanyika katika Kata ya Bwanga, ikihudhuriwa na wananchi, viongozi wa serikali pamoja na wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza katika hafla hiyo, Mbunge Lutandula amesema amelazimika kutumia fedha zake binafsi kununua mitambo hiyo kufuatia kuendelea kuwepo kwa changamoto ya ubovu wa barabara katika jimbo hilo, hali inayochangia ajali na kuathiri shughuli za kiuchumi.

Kwa upande wake, Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu wa CCM Wilaya ya Chato, Dotto Mazuri, amemshukuru Mbunge huyo kwa uamuzi wake wa kununua mitambo hiyo, akieleza kuwa itasaidia kuboresha miundombinu ya barabara na kuchochea maendeleo ya jimbo hilo.

Nao baadhi ya madiwani na wananchi wameelezea furaha yao kwa hatua hiyo, wakisema kuwa mitambo hiyo itasaidia kuondoa changamoto za usafiri na kurahisisha shughuli za kiuchumi.

Wananchi wa Jimbo la Chato Kusini wameeleza kuwa hatua hiyo ni chachu ya maendeleo, wakiamini kuwa upatikanaji wa mitambo hiyo utaimarisha matengenezo ya barabara kwa wakati, kupunguza gharama za usafirishaji, kuongeza usalama barabarani na kuinua shughuli za kiuchumi katika kata na vijiji vya jimbo hilo.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!