Latest Posts

WANANCHI MWIKA WAOMBA MAJI LICHA YA UHARIBIFU WA MIUNDOMBINU YA MAJI KATIKA KIJIJI CHAO

Licha ya kuomba msamaha baada ya kutokea kwa uharibifu wa miundombinu ya maji katika kijiji cha Kiruweni kata ya Mwika Kusini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro,wananchi wa kata hiyo wamezidi kupaza sauti zao na kuomba serikali kuwasaidia kupata huduma ya maji na kuepuka kutumia gharama kubwa kupata huduma hiyo.

Wakiongea katika ziara iliyofanywa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira (MUWSA) Julai 18, 2024 iliyotembelea kata hiyo baada ya uharibifu wa miundombinu yake kutokea na kupelekea mwananchi mmoja kueleza kuwa wanawake wananuka kwa kukosa huduma ya maji, baadhi ya wananchi waliozungumza na Jambo Media katika ziara hiyo akiwemo Eliezer Makyao na Rogasiana wameeleza kuwa uharibifu wa miundombinu umetokea kwa bahati mbaya ila huduma ya maji haikuwepo na haipo katika kata hiyo.

Akiongea kuhusu uharibifu huo mwenyekiti wa kijiji cha Kiruweni Richard Maole ameeleza kuhusu utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa barabara katika kata hiyo unaofanywa kwa ufadhili wa wananchi wa Mwika Kusini waishio nje ya mkoa wa Kilimanjaro uliosababisha miundombinu ya maji kukatwa na kusema kuwa tayari wmaejadiliana na kukubaliana kushiriki kuchangia huduma ya kurejesha miundombinu hiyo.

“Hali ya uharibifu wa miundombinu hiyo siyo uzembe ila ni bahati mbaya ukweli ni kuwa wenye maji ni wachache kutokana na watu kufungiwa bomba na maji hayatoki ” alisema

Naye diwani wa kata hiyo ya Mwika Kusini Denis Pius ameomba radhi kwa uharibifu huo na kueleza kuwa watajadili kuona namna ya kurejesha huduma ya maji.

“Tunaomba radhi kwa uharibifu huu kama alivyo eleza mwenyekiti wa kijiji,tutaona namna ya kushughulikia hili” alirai

Akitoa ufafanuzi wa changamoto hiyo Afisa Mawasiliano na Uhusiano wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Moshi (MUWSA) Flora Nguma amesema ukarabati wa barabara uliofanywa na wanakijiji hao umesababisha kilomita 1.2 za miundombinu ya mabomba kukatwa na kusababisha maji kukatika.

“Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Moshi bado tunafanya jitihada za kuhakikisha kata ya Mwika Kusini inapata maji, tulikuwa tumechimba kisima ndani ya kata hii ili hakikutoa maji na kulitokea changamoto ya uchimbaji na sasa tunampango wa kuchimba kisima kingine kata jirani ya Mwika Kaskazini” Amesema Nguma.

Ameongeza kuwa, MUWSA haitaachia wananchi jitihada za kurudisha miundombinu hiyo, hivyo watashirikiana na ndani ya wiki mbili huduma ya maji itapatikana.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!