Latest Posts

WANANCHI WA KISIWA CHA MAISOME WAPEWA UFAFANUZI WA MABADILIKO YA MSITU NA NAIBU WAZIRI KITANDULA

Naibu waziri wa maliasili na utalii, Dunstan Kitandula amefika katika kisiwa cha Maisome kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa umegwaji wa hekta 2,871.782 kutoka kwenye hifadhi ya msitu wa Maisome ambazo ziliridhiwa na Baraza la Mawaziri kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kibinadamu.

Aidha Kitandula akihutubia mamia ya wananchi katika kambi ya uvuvi Bugombe iliyopo katika kijiji cha Kisaba kata ya Maisome alisema kuwa Wizara imewasilisha rasimu ya Tangazo la Serikali (Notisi ya Kusudio la Kutangaza Mabadiliko ya Eneo la Msitu wa Hifadhi wa Taifa Maisome ya Mwaka 2024) kwenye Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwaajili ya upekuzi ili kukamilisha taratibu za kisheria za mabadiliko hayo.

Akimkaribisha Naibu Waziri wa Maliasili na utalii, Mbunge wa jimbo la Buchosa Erick Shigongo aliishukuru wizara kwa ushirikiano inaoutoa kupitia Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kwani wananchi wamekuwa wakipata misaada mbalimbali kutoka kwa wahifadhi walioko msitu wa hifadhi Maisome na Shamba la Miti Buhindi.

Vilevile Shigongo aliwataka wananchi wanaoishi kwenye kambi ya uvuvi Bugombe kufuata utaratibu uliowekwa pale ambapo wanahitaji kitu au jambo lolote kutoka kwenye hifadhi ya Msitu wa Maisome kwani kwa kufuata utaratibu kutawafanya kufanya shughuli zao za uvuvi kwa tija na ubora wa hali ya juu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!