Latest Posts

WANANCHI WASHAURIWA KUTOKUHIFADHI BARUTI KATIKA MAKAZI YAO

Wananchi wametakiwa kutokuhifadhi baruti katika makazi wanayoishi kutokana na hatari inayoambatana nayo ya kuweza kulipuka inapowekwa katika mazingira yenye moto, joto au umeme.

Hayo yamesemwa na Mhandisi wa mgodi wa Geita Gold Mines (GGM) Katambala Abeli wakati akizungumza na waandishi wa habari katika banda la Chamber of Mines huko Dodoma kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Madini mwaka 2024 katika viwanja vya ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center.

“Baruti ni moja ya nyenzo kuu inayotumika kuvunjia miamba migodini, katika mgodi hauwezi kuvunja miamba mpaka utumie baruti, baruti ina madhara makubwa isipohifadhiwa katika mazingira na hali stahiki kama sheria za nchi zinavyoonesha, haitakiwi kuwekwa pamoja na makazi ya watu kwani inaweza kulipuka” Amesema Katambala.

Amesema kuwa mlipuko mkubwa wa baruti unaweza kusababisha madhara makubwa kwa jamii kama kupoteza maisha, kupoteza viungo na kusababisha uharibifu wa mali na rasilimali nyinginezo, hivyo baruti zinatakiwa zihifadhiwe katika maeneo maalumu yanayoitwa magazini mbali na makazi ya watu ambapo hutengwa kwa kuzungushia fensi au ukuta maalumu.

Amefafanua kuwa eneo lililotengwa kwa kuhifadhia baruti linatakiwa kuwa na vifaa maalumu vya kuzuia milipuko kama radi na wala halitakiwi kuwa na umeme.

Afisa Mahusiano wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji wa Tanzania Chamber of Mines Muki Msami amesema wanatoa elimu ya usalama kazini hasa migodini kwa kutumia wataalamu wa aina mbalimbali walionao.

Msami amesema kazi ya Chemba ya Migodi ni kufundisha jinsi ya kuhifadhi vifaa vya milipuko, kemikali na usalama migodini ili wachimbe madini kwa usalama katika migodi yao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!