Wananchi wa kata ya Nyarugusu jimbo la Busanda mkoani Geita wamemkumbusha kwa mara nyingine tena mbunge wa jimbo hilo, hitaji la jimbo lao kuwa wilaya au kuwa halmashauri Ili kuwarahisishia kupata huduma na kuacha kutembea umbali mrefu kufikia ofisi za halmashauri zilipo.
Akitoa kero hiyo mbele ya mkutano wa hadhara alioufanya mbunge wa jimbo la Busanda Mhandisi Tumaini Magesa katika kijiji cha Nyarugusu, mkazi wa kijiji Daudi Jema amesema wanachoshwa na mzunguko mrefu kufuata huduma ya halmashauri ilioyopo Nzela ambapo wanalazimika kutumia gharama kubwa.
Akijibu swali la hilo Mhandisi Tumaini Magesa amesema tayari Mkoa wa Geita umeshapeleka ombi hilo la kuwa wilaya au halmashauri kwa TAMISEMI na wakasema wanamalizia kwanza kuboresha maeneo ya utawala ya sasa.