Latest Posts

WANAWAKE NA SAMIA GEITA YAWAFARIJI WAJAWAZITO NA KUPANDA MITI HOSPITALI YA RUFAA

Taasisi ya Wanawake na Samia Mkoa wa Geita imefanya ziara maalum katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita, ambapo iliwatembelea wanawake waliojifungua na kuwapatia zawadi mbalimbali.

Pia, taasisi hiyo ilifanya zoezi la kupanda miti katika maeneo ya hospitali hiyo kama njia ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira.

Kaimu Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Mariam Sharifu, amesema shughuli hizo ni sehemu ya matendo ya huruma na upendo kwa jamii, huku pia zikilenga kusherehekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Hatua hii ni ushuhuda wa upendo wa Mama Samia kwa watanzania. Kupitia taasisi yetu, tunajitahidi kufikisha faraja kwa jamii, hususan wanawake walio katika mahitaji maalum,” alisema Sharifu.

Katika tukio hilo, wanawake waliokuwa wamelazwa hospitalini baada ya kujifungua walionyesha furahar kubwa kwa msaada huo. Walimshukuru Rais Dkt. Samia pamoja na Taasisi ya Wanawake na Samia kwa moyo wao wa upendo.

Paulina Majogoro, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Geita, na Winfrida Sakara, mlezi wa Taasisi ya Wanawake na Samia Geita, walihudhuria pia katika tukio hilo na kushiriki katika zoezi la kupanda miti ambapo wamesema wanatambua mchango mkubwa wa Rais Samia katika kuboresha mazingira bora ya wanawake kujifungulia.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Geita, Dk. Mfaume Daudi, alitoa pongezi kwa Taasisi hiyo kwa juhudi zao za kujali ustawi wa jamii na kusaidia katika utunzaji wa mazingira.

“Zoezi hili la kupanda miti ni muhimu sana siyo tu kwa kuboresha mazingira ya hospitali, bali pia kwa kuimarisha afya ya wagonjwa na watumishi wa hospitali hii,” alisema Dk. Daudi.

Taasisi ya Wanawake na Samia imeahidi kuendelea kusaidia jamii kupitia shughuli mbalimbali za kijamii na maendeleo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!