Ikiwa ni siku chache Mkuu wa Nchi Dkt. Samia Suluhu Hassan kufanya ziara kubwa ya siku 5 mkoani Morogoro kukutana na wananchi, kuzindua miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ya viwanda, madaraja, barabara, maabara mtambuka, majengo ya Chuo Kikuu Mzumbe wapinzani Morogoro mjini wameshindwa kuvumilia na kuamua kuhamia Chama cha Mapinduzi.
Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini Abdulaziz Abood amepokea wanachama wapya 320 kutoka vyama mbalimbali vya upinzani walioamua kwa hiyari yao kujiunga na CCM mara baada ya kuridhishwa na kazi nzuri inayofanywa na Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mapokezi hayo yamefanywa tarehe 11.08.2024 katika soko kubwa la matunda na mbogamboga (Soko la Mawenzi) wakati akizindua shina walioanzisha wao la Wakereketwa wa Chama cha Mapinduzi Mawenzi Sokoni.
Akizungumza nao, Mbunge Abood amewakaribisha kwa mikono miwili na kuwapongeza kwa maamuzi yao mazuri ya kujiunga na Chama cha Mapinduzi huku akikubaliana nao kuwa Dkt. Samia amefanya kazi kubwa Nchini na anaendelea kufanya kwa kishindo kikubwa kuwaletea Watanzania maendeleo.
“Mmeshuhudia juzi Rais Samia alikuja Morogoro kututembelea, tumezungumza shida zetu na papohapo akazitatua, tumeomba hospitali ya rufaa katumwagia bilioni 5 palepale, tumemuomba maji mkataba wa bilioni 185 umecheleweshwa kusainiwa kamuelekeza Waziri mpaka oktaba mkataba usainiwe, tumemuomba pesa za barabara, amemuelekeza Waziri atuongezee, hivyo tuna kila sababu ya kumshukuru Rais wetu na ndio maana leo wenzetu uvumilivu umewashinda”