Latest Posts

WASHIRIKI MAFUNZO YA UONGOZI NA USIMAMIZI WA SHULE YALIYOENDESHWA NA ADEM WATAKIWA KUSIMAMIA UFANISI ILI KUINUA UFAULU

 


️23 Septemba, 2024
Shinyanga, Tanzania

Mafunzo ya uongozi na usimamizi wa shule yaliyoendeshwa na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu-ADEM katika Mikoa ya Geita, Kagera, Mwanza na Shinyanga kuanzia tarehe 17 Septemba, 2024 kwa Mkoa wa Geita na Kagera na tarehe 21-23 Septemba, 2024 yamehitimishwa rasmi leo ambapo maafisa elimu katika Halmashauri za Wilaya, Jiji na Manispaa yalipoendeshwa mafunzo hayo wameshiriki hafla za ufungaji wa mafunzo hayo katika halmashauri zao.

Katika Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini Ufungaji Mafunzo umefanywa na Afisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Shinyanga Bw. Andrew M. Mitimba ambaye amewataka walimu wakuu kwenda kusimamia kwa ufanisi ufundishaji na ujifunzaji shuleni ili kuinua ufaulu wa wanafunzi kiwilaya.

Pia amewataka kutoacha umahiri waliojengewa katika kituo cha mafunzo bali kwenda kutekeleza yote kwa vitendo.

Aidha, amewataka kwenda kurithisha maarifa waliyoyapata kupitia mafunzo hayo kwa walimu waliowaacha katika shule zao kupitia programu ya MEWAKA ili wote wawe na umahiri unaotarajiwa.

Kwa upande mwingine, mshiriki wa mafunzo hayo ametoa shukrani kwa ADEM kupongeza namna washiriki wameyapokea mafunzo hayo kwa njia ya utenzi kama inavyoonekana katika video hapo juu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!