Latest Posts

WASIRA: NCHI INAKOPA KWA MAENDELEO YA KIZAZI CHA SASA NA KIJACHO

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Wasira, amesema kuwa mikopo inayochukuliwa na serikali ni kwa ajili ya maendeleo ya muda mrefu ambayo yatawanufaisha Watanzania wa sasa na vizazi vijavyo.

Amesema kuwa deni la taifa la shilingi trilioni 97 si kwamba limekopwa lote na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, bali ni deni ambalo limekuwa likiongezeka kwa miaka mingi tangu enzi za Rais wa Kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Wasira alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM katika Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu, kwenye kikao cha ndani kilichokuwa sehemu ya ziara yake ya kikazi mkoani humo. Ziara hiyo inalenga kukagua uhai wa CCM, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, na kusikiliza kero za wananchi.

“Tunakopa ili kufanya jambo ambalo tutaishi nalo kwa miaka mingi. Faida zake zitawanufaisha kizazi cha sasa na hata kijacho. Deni hili si kwamba amekopa Rais Samia trilioni 97, bali limekuwepo kwa muda mrefu na linajumuisha madeni ya zamani ambayo Tanzania ilianza kulipa baada ya miaka 40,” amesema Wasira.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!