Latest Posts

WATAFITI KUTOKA NCHI TATU KUFANYA TAFITI ZA STADI ZA MAISHA NA MAADILI KWA WATOTO

Washirika wa kikanda kutoka Tanzania, Kenya na Uganda wamekutana nchini Tanzania kujadili kwa kina mbinu bora za kufanya tafiti za stadi za maisha na maadili kwa watoto wenye umri wa miaka 13 hadi 17.

Akizungumzia programu ya kukuza stadi za maisha na maadili (Alive) iliyowakutanisha watafiti kutoka nchi hizo tatu wilayani Hai mkoani Kilimanjaro Januari 22, 2026 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Uwezo Tanzania, Baraka Mgohamwende amesema kuwa programu hiyo ni juhudi ya kikanda inayosaidia mifumo ya elimu ya nchi hizo kukuza, kufundisha, kutafiti na kutathimini maadili na stadi za maisha zinazowawezesha wanafunzi kufanikiwa shuleni na katika maisha kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Zizi Africque amesema kuwa watoto wengi hawajafikia kiwango ambacho kinahitajika kwa stadi za maisha ambapo asilimia kumi pekee ya vijana walio katika umri wa miaka 13 hadi 17 ndio wanaonesha kiwango cha ustadi kinacho faa kwa umri huo.

Naye Glory Mbwambo, Kaimu Mthibiti Mkuu Ubora wa Shule Mkoa wa Kilimanjaro anayesimamia Manispaa ya Moshi amesema kuwa changamoto ya ndoa kuvunjika na malezi ya mzazi mmoja kunasababisha watoto kukosa stadi za maisha na maadili hivyo uwepo wa mashirika hayo kunasaidia Serikali kufika maelengo ya kuwa na watoto wenye stadi za maisha na maadili.

 

Programu hiyo ya Alive inatekelezwa kupitia ushirikiano wa pamoja unaojumuisha Uwezo Tanzania, Uwezo Uganda, Zizi Africque, OCODE na Milele Zanzibar, kwa kushirikiana na washirika wa kitaaluma wakiwemo Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Chuo Kikuu Cha Luigi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!