Latest Posts

WATALII ELFU 32 WATEMBELEA HIFADHI YA TAIFA SAADANI,MAPATO YAFIKIA BILIONI 2.5

Watalii takribani elfu 32 hutembelea  hifadhi ya taifa saada kwa kipindi cha mwaka ambapo shughuli za utalii katika hifadhi hiyo zimefanikiwa kuzalisha zaidia ya shilingi Bilioni 2 kwa mwaka wa fedha wa 2024/25.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Hifadhi ya Saadani, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Gladys Ng’umbi, amesema kuwa takwimu za watalii wanaotembelea Zaidi hifadhi ya Taifa ya  saadani ni watalii elfu 19,500 wakiwa ni watalii wa ndani  huku watalii wa nje wakiwa ni elfu 11,000 ambapo kwa ujumla hifadhi hiyo hupokea watalii elfu  32,000 kwa mwaka.

“kwasasa mapato yanaendelea kuongezeka ambapo kwa mwaka wa fedha uliopita  tulipata jumla ya mapato Bilioni 2.5 ambayo yalitokana na shughuli za utalii katika hifadhi ya taifa ya saadani kwaiyo tunaamini kabisa kutokana na juhudi za Rais wa Jamuhri ya Muungano wa Tanzania mapato haya yataongezeka kwani amekuwa kinara mkubwa katika kutangaza utalii hapa nchini’’

kwaupande wake KATIBU Tawala Mkoa wa Tanga, Rashid Mchatta amesema kuwa watumishi  wa umma kufanya utalii wa ndani ni fursa ya kujifunza mambo mbalimbali na kuona fursa zilizopo kwenye sekta ya utalii.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!