Mwalimu Kiongozi wa huduma ya matengenezo ya kiroho Augustine Tengwa ameviomba vyama vya siasa nchini kutogombania madaraka kuilinda amani ya Tanzania
Ametoa kauli hiyo Oktoba 11 Jijini Dar es salaam wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maono ambayo watumishi wamefunuliwa kuelekea uchaguzi kuwa kutakuwa tishio la kiusalama kama hakutachukuliwa hatua kuzuia hali hiyo.
“Tuilinde amani tuliyonayo hatujawahi kuwa wakimbizi kama mataifa mengine ya jiran tusije kuwakama Rwanda, Kenya, Libya, Ukraine na Israel na hamas”, amesema Mch. Tengwa
Kwa upande wake, Mtumishi wa Mungu Agness Bruno amewaasa Watanzania kurudi kuwa taifa moja na wamoja kwa kujua thamani ya kila Mtanzania ili kuepusha umwagaji damu.
Naye mtumishi mwingine, Alpha Kiamba amewaasa Watanzania kutopuuza taarifa kutoka kwa watumishi wa Mungu hasa maono bali kuyapokea na kufanyia maombi
Akitolea mfano maporomoko ya mlima Hangang na mafuriko ya Rufiji amesema hayo yalikuwa maono kutoka kwa watumishi na hilo la uchaguzi lisipuuzwe.