Latest Posts

WATENDAJI KATA WATAKIWA KUWATOE HOFU WANANCHI KAULI YA ‘KALISAIDIE JESHI LA POLISI’

Watendaji wa kata wametakiwa kwenda kutoa elimu na kuondoa thana potofu iliyojengeka vichwani kwa wananchi kuhusiana na kauli ya ‘Kalisaidie Jeshi la Polisi’ kuwa ina lengo zuri la kusaidia uchunguzi.

Akitoa elimu ya ulinzi na usalama kwa viongozi na wataalamu wa ngazi za Wilaya ya Kwimba na Mamlaka za Serikali za Mitaa, Mkufunzi wa Elimu ya Uraia na Utawala Bora kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani, ASP Iddah John Ringo amesema kauli hiyo haimaanishi mtoa taarifa anawajibika kwa tukio hilo bali hulenga kulisaidia Jeshi la Polisi kufanikisha uchunguzi.

Amesema wakati mwingine Jeshi la Polisi hupata taarifa kwa mara ya kwanza ambazo hazijajitosheleza hivyo mtoa taarifa hutakiwa tena kwenda kituo cha Polisi kutoa taarifa zaidi.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Kwimba, Ng’wilabuzu Ludigija amewataka washiriki kwenda kufanyia kazi kile walichojifunza ili kuwa na utawala bora.

Wakiipongeza Serikali kwa mafunzo hayo Mtendaji wa Kata ya Nkalalo, Salum Mussa Salum na Mtendaji wa Kata ya Marietha Mushi wameahidi kwenda kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama huku wakiahidi kutoa elimu ya ulinzi na usalama kwa wananchi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!