Latest Posts

WATOTO 361 SERENGETI WAPEWA MAHITAJI MUHIMU KUANZA KIDATO CHA KWANZA.

Taasisi isiyo ya kiserikali ya Nyansaho Foundation iliyoasisiwa na Dkt. Rhimo S. Nyansaho, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge jimbo la Serengeti imegawa mahitaji ya muhimu ya shule kwa wanafunzi 361 walioshindwa kujiunga kidato cha kwanza kwa kukosa mahitaji ya msingi!

Mratibu wa Nyansaho Foundation Bi. Modesta Mwema amesema taasisi hiyo itaendelea kuwa daraja la maendeleo Serengeti, Kanda ya Ziwa na taifa kwa ujumla katika Elimu, Afya na Mahitaji Maalumu!

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Serengeti, Mary Daniel Joseph, ameabainisha kuwa ni 76% tu ya wanafunzi waliofuzu kwenda kidato cha kwanza 2026 ndio waliokwisha kuripoti shule huku akitoa rai kwa wadau wengine wa maendeleo kuiga mfano wa Nyansaho Foundation ili kusaidia watoto wengi nchini kuendelea na masomo ngazi mbalimbali za elimu.

Wazazi na wanafunzi wamefarijika na kuishukuru taasisi hiyo kwa kuwasaidia madaftari, sare za shule, mabegi, viatu, kalamu, rula, karatasi nyeupe na mahitaji mengineyo yatakayowawezesha kuendelea na masomo ya sekondari.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!