Latest Posts

WATOTO WA MITAANI KILIMANJARO: MIGOGORO YA FAMILIA NA MILA POTOFU YATAJWA KUWA CHANZO

Migogoro ya kifamilia, ukatili wa kijinsia, vifo, mirathi na mila potofu zimetajwa kama sababu kuu zinazochangia watoto kuendelea kuishi na kufanya kazi mtaani katika jamii nyingi hapa nchini.

Kauli hiyo imetolewa Aprili 11, 2025 na Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Godfrey Mnzava, alipomwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kwenye Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto Anayeishi na Kufanya Kazi Mtaani. Maadhimisho hayo yamefanyika katika viwanja vya Soko la Manyema, Manispaa ya Moshi, yakiandaliwa na Shirika la Amani Center for Street Children, sambamba na uzinduzi wa kampeni ya msaada kwa watoto hao.

Mnzava amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano kwa taasisi na mashirika yanayosaidia watoto wa mtaani ili kuhakikisha wanatimiza ndoto zao na kurejeshwa kwenye familia zao salama.

“Jamii nayo ina jukumu kubwa la kushiriki kutokomeza sababu zinazopelekea watoto kukimbilia mtaani. Tushirikiane kuhakikisha watoto wanakuwa salama katika mazingira yao,” alisema DC Mnzava.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Amani Center, Daniel Temba, amesema mwaka 2024 walifanikiwa kuwakomboa watoto 164 waliokuwa mitaani na kuwaweka katika nyumba salama huku wengine wakirudishwa kwa familia zao.

Ameongeza kuwa mwingiliano wa mipaka na fursa nyingi za kiuchumi Mkoani Kilimanjaro vimekuwa kichocheo cha watoto wengi kutoka maeneo mbalimbali, hata kutoka nchi jirani, kuingia mjini kwaajili ya kujitafutia kipato na kuishia mitaani.

Maadhimisho hayo yameambatana na kauli mbiu ya mwaka huu isemayo: “Imarisha Ushirikiano, Kuzuia Watoto Kuishi na Kufanya Kazi Mtaani.”

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!