Latest Posts

WATU 566 WAKUTWA NA UGONJWA KWENYE MFUMO WA CHAKULA NJOMBE

 

Wagonjwa zaidi ya 23,000 wamepatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa mkoa wa Njombe huku wagonjwa wa dharura na mahututi wakiwa 1,322 katika kipindi cha mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu.

Hayo yameelezwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa mkoa wa Njombe Dk. Gilbert Kwesi katika uzinduzi wa huduma ya uchunguzi wa magonjwa ya mfumo wa chakula (ENDOSCOPY UNIT) uliofanyika katika hospitali hiyo.

Dk. Kwesi amesema magonjwa hayo ya mfumo wa chakula mchanganyiko yamekuwa yakiongoza kwa kuwa na idadi ya wagonjwa wengi ambapo kwa kipindi cha Januari hadi Septemba wagonjwa 566 wamefanyiwa uchunguzi na kutibiwa.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka mara baada ya kuzindua huduma hiyo amewataka watumishi wa hospitali kuendelea kutoa huduma bora sambamba na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma.

“Fanyeni kazi kwa kuzingatia maadili lakini tembeeni kifua mbele kwa sababu serikali inaendelea kuhakikisha mnafanya kazi katika mazingira rafiki na kuridhisha pamoja na kutatua matatizo yenu ya kimaslahi,” amesema Mtaka.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!