Latest Posts

WAWEKEZAJI WATANZANIA WATAKIWA KUWEKEZA KARAGWE KAGERA, KILIMO NA MIFUGO VYAPEWA KIPAUMBELE

Mkuu wa Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, Julius Laizer amewataka wawekezaji hasa wa ndani kwenda kuwekeza wilayani humo ambapo kuna eneo limetengwa lenye ukubwa wa hekta 2,000 kwa ajili uwekezaji wa viwanda.

Laizer amesema hayo Julai 15, 2024 alipotembelewa na maafisa kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) waliopo kwenye kampeni ya kuhamasisha uwekezaji wa ndani kwa awamu ya pili sasa ikiwa ni mwendelezo wa kukamilisha kupita mikoa yote ya Tanzania.

Amesema Wilaya ya Karagwe ina fursa nyingi za uwekezaji hasa katika kilimo na mifugo na ina uhitaji wa viwanda vya nyama, dawa za mifugo pamoja na viwanda vya kahawa.

“Kupitia TIC kwa jitahada hizi za kuhamasisha uwekezaji naamini kabisa kutaleta wawekezaji na kuisaidia Kagera kuinuka kiuchumi” Amesema Laizer.

Aidha, Laizer ametoa rai kwa TIC kutoa elimu na kuweka mazingira rahisi zaidi kwa wawekezaji wa ndani ili kuchochea kasi ya uwekezaji na kuwawezesha kusajili miradi yao.

Katika jitihada za kuhamasisha uwekezaji wa ndani, TIC inatembelea miradi mbalimbali na kutoa elimu kwenye mikoa ya Kagera, Mwanza, Mara, Simiyu, Lindi, Ruvuma, Rukwa, Kigoma na Katavi, na inashirikiana na Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) kwa upande wa Unguja na Pemba.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!