Latest Posts

WAZAZI NA WALEZI WATAKIWA KUSIMAMIA ELIMU KWA WATOTO

Jumla ya tani 125,169 za korosho ghafi zimesafirishwa kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) mkoani Mtwara na tani elfu 30,000 zimepakiwa kwenye makasha kwa ajili ya kusafirishwa kwenye bandari hiyo.

Usafirishaji huo umetokana na kuboreshwa kwa miundombinu ya bandari hiyo ya Mtwara iliyogharimu kiasi cha Shilingi bilioni 157.8.

Hayo ameyaeleza Mkuu wa Wilaya ya Newala Alhaji Rajabu Kundya kwenye sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambapo kwa mkoa wa Mtwara, sherehe hizo zimefanyika kata na kijiji cha Makukwe kwenye halmashauri ya Mji Newala na kusema kuwa mkoa huo ni miongoni mwa mikoa iliyofanikiwa kwa kuongeza wigo katika nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, afya, usafirishaji na nishati.

Aidha kwa upande wa sekta ya afya kiasi cha Shilingi bilioni 15.6 kimekamilisha ujenzi wa hospitali ya rufaa Kanda ya Kusini na kuanza kutoa huduma, na Shilingi bilioni 6 zimetumika kwa ajili ya ujenzi wa vituo vipya 12 vya kutolea huduma za dharula za uzazi.

Pia amewataka wazazi na walezi kuongeza jitihada za kuhakikisha wanasimamia elimu kwa watoto ili watoto hao wawe sehemu ya mafanikio hayo kwani serikali imetoa bilioni 4 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa shule ya wasichana ya kitaifa inayojengwa Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu

Sambamba na hilo amewasihi viongozi waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliyofanyika Novemba 27, 2024 kuhakikisha wanawashirikisha watu wote katika uongozi wao kwani maendeleo yanahitaji kila mtu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Newala, Yusuphu Kateule amewataka vijana kuchangamkia uhuru kwa kujifunza mambo mbalimbali yaliyofanyika kabla na baada ya uhuru ili kuongeza ubunifu katika kila nyanja kwa kuzingatia kanuni, sheria na taratibu husika.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!