Latest Posts

WAZAZI WAHOFIA WATOTO KUTEKWA BAADA YA NOAH NYEUSI KUONEKANA SHULENI MBURAHATI

Baadhi ya wazazi na walezi wenye watoto katika shule ya msingi Mburahati iliyopo katika mkoa wa Dar es Salaam wamefika shuleni hapo mchana wa Julai 22, 2024 kwa lengo la kuwafuata watoto wao kutokana na hofu iliyotanda ikidaiwa kuna watu wana nia ya kuwateka hasa baada ya kufahamu uwepo wa gari linalozunguka katika viunga na viwanja vya karibu na shule hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa JamiiForums, inadaiwa kulitokea gari aina ya Noah nyeusi ambayo haina namba iliyokuwa karibu na maeneo ya shule, hali hiyo ikawashtua baadhi ya watu na kuanza kupeana taarifa juu ya uwepo wa gari hiyo ambayo baada ya muda iliondoka.

Baada ya taarifa hiyo kusambaa wazazi na walezi wakakusanyika eneo la shule wakitaka kujua kama watoto wao wapo salama, wakazuiwa getini hata hivyo idadi ilipoongezeka uongozi wa shule ukaita Jeshi la Polisi kusaidia kuwatuliza wazazi na walezi.

Jeshi la Polisi lilianza kuwatoa watoto wakitumia kipaza sauti na spika kuita majina yao kisha mzazi au mlezi alitakiwa kuingia ndani kuthibitisha uwepo wa mtoto wake na baada ya kuthibitisha aliondoka na mwanaye. Watoto ambao hawakuwa na watu waliokuja kuwachukua wakalazimika kubaki shuleni kwa muda.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!