Latest Posts

WAZAZI WATAKIWA KUACHA KUWASHAWISHI WANAFUNZI KUTOFANYA VIZURI KWENYE MITIHANI YAO

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala Julai 23,2024 amefanya ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo sekta ya elimu na afya lengo ni kujionea kama miradi yote ya mwaka wa fedha 2023/24 imekamilika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara.

Akiwa katika ziara hiyo, mkuu huyo wa mkoa amewataka wazazi kuacha kuwashawishi wanafunzi kutofanya vizuri kwenye mitihani yao na badala yake wawe mstari wa mbele kuhakikisha wanafanya vizuri ili kutengeneza viongozi wazuri wa mkoa na taifa la badaye.

“Niwaombe wazazi wasiwe chanzo cha kuwashawishi wanafunzi kutofanya vizuri kwenye mitihani yao, badala yake wawe chanzo kizuri cha ufuatiliaji wa watoto ili waweze kufanya vizuri katika masomo na tutengeneze viongozi wazuri wa kesho kwa ajili ya mkoa na taifa letu kwa ujumla” Amesema Sawala.

Aidha amewapongeza Halmashauri ya Manispaa hiyo kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa miradi na kuwataka kuongeza kasi ili wananchi waweze kuona matokeo ya kazi nzuri ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Katika hatua nyingine, ametoa rai kwa wanafunzi na walimu kwenye Manispaa hiyo kutunza miundombinu ya shule na thamani kwa ujumla ili iendelee kudumu kwa muda mrefu, na kuzingatia masomo ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani yao ikizingatiwa serikali imewekeza fedha nyingi kwenye sekta hiyo ya elimu.

Miradi ya elimu aliyotembelea ni pamoja na ujenzi wa bwalo na jiko kwenye shule ya sekondari Naliendele, na matundu ya vyoo nane na ujenzi wa madarasa Matano katika shule ya sekondari ya wasichana ya Mtwara Girls.

Miradi mingine ni ujenzi wa madarasa mawili na ujenzi wa matundu sita ya vyoo katika shule ya msingi Magomeni, madarasa matatu na matundu sita ya choo ya shule ya msingi Rahaleo, na vyumba vinne vya madarasa, ofisi mbili za walimu na matundu saba ya vyoo katika shule ya sekondari Ufundi Mtwara hivyo kufanya jumla ya gharama ya miradi yote kuwa zaidi ya Shilingi bilioni 1.5.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!