Latest Posts

WAZIRI BASHUNGWA AWATAKA WAHANDISI KUENDANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA YA AKILI MNEMBA

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ametoa wito kwa wahandisi nchini kuhakikisha wanajiendana na kasi ya mabadiliko ya teknolojia, hususan teknolojia ya Akili Mnemba (Artificial Intelligence – AI), ili kutatua changamoto mbalimbali zinazokabili jamii.

Bashungwa ameyasema hayo Septemba 5, 2024, wakati akifungua Maadhimisho ya 21 ya Siku ya Wahandisi, yaliyokuwa na kauli mbiu isemayo: “Kuandaa Nguvukazi ya Uhandisi katika Zama za Akili Mnemba – Mafunzo na Kuimarisha Ujuzi wa Watalaam wa Kada ya Uhandisi”.

“Tumieni fursa hii kutafakari changamoto mbalimbali za shughuli za kihandisi zenye mahusiano ya moja kwa moja na maendeleo ya nchi yetu, badilishaneni mawazo na kuona ni teknolojia ipi itasaidia kutatua changamoto”, amesema Bashungwa.

Aidha, Bashungwa amehimiza Wakala wa Barabara (TANROADS) kutoa nafasi kwa Wakandarasi na Washauri Elekezi wazawa kushiriki katika ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa na mvua za El-Nino.

Serikali tayari imetenga kiasi cha shilingi bilioni 840 kwa ajili ya kurejesha madaraja na makalvati yaliyoharibika. Waziri Bashungwa alisisitiza umuhimu wa kuwapa vijana nafasi za mafunzo kwenye miradi hiyo, ili kuwajengea uwezo wa kitaalamu.

“Hakikisha kila mradi unachukua wanafunzi wawili katika miradi 114 ya kurejesha miundombinu iliyoyahiribiwaa mikoa yote nchini, hii itasaidia kuinua vijana na kuwajengea uwezo”, amesema Bashungwa.

“Hakikisha kila mradi unachukua wanafunzi wawili kutoka kwenye miradi 114 ya kurejesha miundombinu iliyoathiriwa nchi nzima. Hatua hii itasaidia kuinua vijana na kuwapa uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi,” ameongeza Bashungwa.

Bashungwa ametoa rai kwa wahandisi na wataalam wote wazawa kujiamini na kufanya kazi kwa uaminifu, Kizalendo, kukamilisha miradi kwa wakati na kuzingatia miiko na viapo vya kihandisii walivyoapa ili kuepusha masuala ya ongezeko la gharama katika miradi na miradi kuharibika kabla ya wakati.

Katika hotuba yake, Bashungwa alitoa maagizo kwa TANROADS kuhakikisha wanapitia usanifu wa miradi kabla ya kutangaza zabuni, hasa kwa miradi ambayo usanifu wake umefanyika miaka mingi iliyopita ili kuhakikisha viwango bora vinafuatwa.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Aisha Amour, amebainisha kuwa serikali inatenga Shilingi milioni 788 kila mwaka kwa ajili ya kugharamia mafunzo ya wahandisi wahitimu kupitia mpango wa Structured Engineers Apprenticeship Program (SEAP). Mpango huu unalenga kuwaongezea wahandisi hao ujuzi wa kipekee katika sekta ya uhandisi.

Msajili wa Bodi ya Usajili ya Wahandisi (ERB) Mhandisi Bernad Kavishe, ameeleza kuwa hadi kufikia Julai 31, 2024, jumla ya wahandisi 39,236 wamesajiliwa nchini Tanzania. Kati ya hao, wahandisi wanawake ni 5,276, mafundi sanifu 2,976, kampuni za ushauri wa kihandisi 431, na maabara za uhandisi 52.

Maadhimisho ya mwaka huu yamehudhuriwa na wahandisi takriban 4,000, huku wahandisi zaidi ya 300 wakila kiapo cha utii wa uhandisi, hatua inayoonesha umuhimu wa maadili katika taaluma hiyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!