Latest Posts

WAZIRI MKUU AAGIZA BIDHAA ZA AFYA ZIKIDHI VIWANGO, AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA OKSIJENI

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa ameziagiza taasisi za kudhibiti viwango nchini kuhakikisha bidhaa zote zinazozalishwa, hususan za afya, zinakidhi ubora unaotakiwa ili ziweze kushindana katika masoko ya kimataifa.

Ametoa agizo hilo, Alhamisi Machi 20, 2025, baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mitambo ya kuzalisha oksijeni kwa matumizi ya hospitali katika ofisi za TOL Gases, Temeke, Dar es Salaam. Amesisitiza kuwa ni muhimu kuhakikisha soko linakuwa na bidhaa salama, bora, na zinazokubalika kimataifa.

Majaliwa amesema mradi huo, utakapokamilika mwaka 2026, utaweza kuzalisha lita milioni 4.1 za oksijeni ya matibabu kwa mwaka, hatua inayotarajiwa kuboresha upatikanaji wa gesi hiyo katika hospitali na vituo vya afya nchini. Aidha, amesema mradi huo utapunguza gharama za oksijeni kwa asilimia 35, hivyo kusaidia kuimarisha huduma za afya kwa wananchi.

“Mradi huu utaongeza upatikanaji wa oksijeni katika hospitali na zahanati nchini na kupunguza vifo vitokanavyo na magonjwa ya kupumua, ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vya akina mama na watoto,” amesema Waziri Mkuu.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godfrey Mollel, amesema oksijeni inayozalishwa kwa njia hii itakuwa na viwango vya ubora vinavyotakiwa, hivyo kusaidia kuboresha huduma za afya na kupunguza vifo.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TOL Gases, Daniel Warungu, ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kujidhatiti katika kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa Watanzania.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!