Latest Posts

WAZIRI MKUU AWATAKA WAKULIMA KUTUMIA NANENANE KUJIFUNZA TEKNOLOJIA

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka wakulima, wajasiriamali na wafanyabiashara kutumia fursa ya Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa ya Nanenane 2024 kujifunza teknolojia mbalimbali za kilimo zitakazowawezesha kulima kisasa na kuzalisha zaidi.

Amesema hayo tarehe 1 Agosti, 2024 alipofungua Maonesho hayo ambayo kitaifa yanafanyika katika viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.

Waziri Mkuu amesema amefurahishwa na ushirikiano mzuri wa Sekta ya Kilimo, Na Sekta ya Mifugo na Uvuvi katika kuhakikisha washiriki wanajifunza teknolojia za kisasa na mbinu mbalimbali za kuinua kiuchumi shughuli za kilimo.

Ameeleza kuwa wakulima pia watajifunza matumizi ya zana bora za kilimo, matumizi ya mbegu bora na upimaji wa afya ya udongo ili kuwa na kilimo kwa uhakika na si kwa kubahatisha.

Maonesho ya Nanenane 2024 yanafanyika katika kanda saba nchini ambazo ni Nyanda za Juu Kusini jijini Mbeya kwenye Uwanja wa John Mwakangale, Kanda ya Mashariki mjini Morogoro kwenye Viwanja vya Mwl. Julius Kambarage Nyerere, Kanda ya Kusini mjini Lindi kwenye Viwanja vya Ngongo, Kanda ya Ziwa Magharibi jijini Mwanza katika Viwanja vya Nyamhongolo, Kanda ya Ziwa Mashariki  mkoani Simiyu katika Viwanja vya Nyakabindi, Kanda ya Kaskazini jijini Arusha kwenye Viwanja vya Themi, na Kanda ya Magharibi mjini Tabora kwenye Viwanja vya Fatma Mwasa.

Kauli mbiu ya Maonesho ya Kilimo ya Kimataifa Nane Nane 2024 ni “Chagua Viongozi Bora wa Serikali za Mitaa kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi”.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!