Latest Posts

WAZIRI MWIGULU AWASIHI WATANZANIA KUTUMIA BIDHAA ZA NDANI KUJENGA UCHUMI WA TAIFA

Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka Watanzania kuunga mkono juhudi za kujenga uchumi wa ndani kwa kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini, badala ya kutegemea bidhaa za nje.

Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo Jumamosi tarehe 31 Agosti 2024, jijini Dodoma, wakati akifungua mkutano kuhusu sheria ya ununuzi wa umma, sheria ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi, pamoja na matumizi sahihi ya takwimu kwa Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, na Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya.

“Tuna viwanda vingi vilivyojengwa hapa nchini vinavyozalisha vifaa vya ujenzi na vinavyolipa kodi hapa hapa kwetu. Hata hivyo, sheria na zabuni zetu zilizopita zilikuwa zikitoa upendeleo kwa bidhaa za nje, hali iliyonyima fursa viwanda vyetu vya ndani kukua,” alisema Dkt. Mwigulu.

Aidha, amewashauri wananchi kuacha tabia ya kulalamika mitandaoni, akitoa mfano wa jinsi watu wanavyotoa maoni yasiyofaa anapoposti picha za chipukizi wake, wakimkosoa kuwa anakula fedha za kigeni (dola).

“Fikiria tunapompa mkandarasi kutoka nje zabuni ya ununuzi wa vifaa vya ujenzi, halafu baadaye Dola inakuwa adimu, mnaiuliza serikali. Inashangaza kuona kwamba naposti tu picha ya kumtakia mwana wangu wa chipukizi heri ya kuzaliwa, na watu wanaanza kusema ‘ameshiba dola zetu.’ Wanajiuliza anakutana nazo wapi?”, amehoji Mwigulu.

Katika hotuba yake, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI Dkt. Festo Dugange aliongeza kuwa kuna changamoto kubwa katika eneo la ununuzi wa umma, na aliwataka viongozi hao kutumia mafunzo hayo kuboresha mipango yao kwa kutumia takwimu sahihi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!