Latest Posts

WAZIRI SIMBACHAWENE AELEKEZA NAMNA BORA ZAIDI YA KUSHUGHULIKIA MASUALA YA KIUTUMISHI IKIWEMO BARUA ZA AJIRA MPYA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amemuelekeza Katibu Mkuu- Utumishi, Bw. Juma Mkomi kuhakikisha barua za walioshinda usaili na kupangiwa vituo vya kazi zinatolewa kwenye mikoa husika walikofanyia usaili badala ya kuwalazimu kusafiri hadi jijini Dodoma kufuata barua hizo.
 
Simbachawene, ametoa maelekezo hayo Machi 29, 2025, jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
 
Waziri Simbachawene ameonesha kutoridhishwa na mfumo wa sasa unaowalazimu watumishi wapya kusafiri hadi Dodoma kupata barua zao hata kama wamepangiwa kufanya kazi katika mkoa walikofanyia usaili.
 
“Unakuta mtumishi amefaulu usaili Kigoma, anasafiri Dodoma kuchukua barua, kisha anarudi Kigoma au anakwenda Lindi. Hii ni hasara kwa taifa na mzigo kwa mtumishi mwenyewe,” amesema.
 
Amesisitiza kuwa barua za ajira zitatolewa kwenye Ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa walikofanyia usaili, badala ya kuwategemea watendaji wa Sekretarieti ya Ajira pekee.
 
Katika hatua nyingine, Waziri Simbachawene ameagiza kuanzishwa kwa “One Stop Centre” ndani ya Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora jijini Dodoma. Kituo hicho kitalenga kusikiliza na kutatua changamoto za watumishi wa umma papo kwa papo bila kuwalazimu kurudi mikoani kwa marekebisho ya taarifa zao za kiutumishi.
 
“Tunataka mahali ambapo mtumishi wa umma akifika na tatizo lake, linatatuliwa hapo hapo. Kituo hiki kitakuwa na maafisa waandamizi wa kada zote pamoja na wanasaikolojia wa kusaidia mtumishi yeyote mwenye changamoto,” amesema Waziri.
 
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. Juma Mkomi, amepongeza maelekezo ya Waziri na kuahidi kuyatekeleza kwa ufanisi na weledi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!