Latest Posts

WAZIRI WA ZAMANI AIKOKOTA UHAMIAJI MAHAKAMANI, KESI KUSIKILIZWA LEO

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam leo, Ijumaa Januari 23.2026, inatarajiwa kusikiliza maombi Na. 488/2026 yaliyofunguliwa na Waziri wa zamani Geoffrey Idelphonce Mwambe dhidi ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji (CGI) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG)

Katika maombi hayo yaliyopo mbele ya Jaji David Ngunyale yanayotarajiwa kusikilizwa saa 04:00 asubuhi, mleta maombi (Geoffrey Idelphonce Mwambe) anaiomba Mahakama impe kibali cha kufungua kesi ya msingi ya kuishtaki Jamhuri kufuatia Idara ya Uhamiaji kunyang’anya ‘passport’ sita (6) za familia yake, yaani ‘passport’ zake binafsi mbili (2), moja (1) ya mkewe na nyingine za watoto wake

Mwambe ambaye inaelezwa kuwa kwa sasa ni mgonjwa, awali alitarajia kusafiri kuelekea nje ya nchi (Ujerumani) kwa ajili ya matibabu, lakini alipofika kwenye mpaka wa Namanga akiwa ameambatana na familia yake, ghafla alishangazwa kuona anazuiliwa kusafiri na maafisa wa Uhamiaji wanagoma kurudisha ‘passport’ bila kutoa maelezo ya kina

Mwanzoni, maombi hayo ambayo yamefunguliwa kwa hati ya dharura yalitajwa Mahakamani hapo Januari 20.2026 mbele ya Naibu Msajili wa Mahakama Levin Lyakinana, ambapo Mwambe anawakilishwa na Mawakili Mpale Mpoki na Hekima Mwasipu, wakati upande wa wajibu maombi jopo lake likiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi Daniel Nyakia

Ikumbukwe kuwa, Geoffrey Idelphonce Mwambe ambaye ni Mbunge wa zamani wa Jimbo la Masasi, Mkoani Mtwara (CCM) pia amewahi kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara katika Serikali ya Awamu ya Tano iliyokuwa inaongozwa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji mwanzoni mwa Serikali ya Awamu ya Sita iliyoko chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Aidha, katika safari yake ya uongozi ameshika nafasi mbalimbali serikalini ikiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa kilichokuwa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Mkuu wa Wilaya

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!