Latest Posts

WIKI YA MAMA YAZINDULIWA KUADHIMISHA MIAKA MINNE YA RAIS SAMIA

Katika kuadhimisha miaka minne ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Kampeni ya Mama Asemewe imezindua rasmi Wiki ya Mama katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Youth Park, jijini Dar es Salaam.

Uzinduzi huo umefanywa Machi 16, 2025 na Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama Asemewe Taifa, Geofrey Kiliba ambaye amesisitiza umuhimu wa kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazotekelezwa na Rais Samia.

Katika hotuba yake, Kiliba ameeleza kuwa kwa kipindi cha siku saba za maadhimisho, wanakampeni wa Mama Asemewe watakuwa wakizungumzia mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia. Aidha, shughuli hizo zitahitimishwa kwa maazimio ya wasomi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, ambapo wanavyuo watatoa mwelekeo wa namna ya kuendelea kumuunga mkono Rais kwa maendeleo ya Tanzania.

Maadhimisho hayo yalianza kwa matembezi ya wanavyuo takribani 3,500, wakipaza sauti za kumuunga mkono Rais Samia kupitia kampeni yao ya Mama Asemewe. Matembezi hayo yalikusudia kusambaza ujumbe kuhusu hatua za maendeleo zilizofikiwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake.

Mbali na matembezi, uzinduzi huo ulitanguliwa na mashindano ya mpira wa miguu yaliyopewa jina la Mama Asemewe Cup, ambapo timu mbalimbali kutoka vyuo na taasisi za elimu ya juu jijini Dar es Salaam zilishiriki. Katika mashindano hayo, Timu ya Chuo cha LITA iliibuka mshindi wa kwanza na kutunukiwa zawadi ya shilingi 700,000, Timu ya Chuo cha CBE pamoja na Jogging Club ya Temeke zilishika nafasi ya pili, kila moja ikipata zawadi ya shilingi 400,000

Zawadi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Samia for Us, Alawi Abdallah Rwegoshora, ambaye amesisitiza kuwa Mama Asemewe itaendelea kuwa jukwaa la kuelimisha jamii kuhusu maendeleo ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia.

Wiki ya Mama inaendelea kwa shughuli mbalimbali za kijamii, mijadala ya kitaaluma, na vikao vya tathmini ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, huku wasomi wakijipanga kwa maazimio muhimu kuelekea uchaguzi wa 2025.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!