Katika kipindi cha miezi sita ,Wilaya ya Hai imefanikiwa kusajili wagonjwa wanaotumia dawa za VVU kwa asiliamia 98 kwakutumia alama za vidole ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa hao na kutunza taarifa zao ikiwa watahama au kuchukulia dawa sehemu nyingine.
Hayo yameelezwa na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Hai Daktari Emmanuel Minja katika Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo baada ya Diwani wa Kata ya Masama Kusini Cedrick Pangani ambaye ni mjumbe wa Kamati ya UKIMWI kushauri elimu ya utolewaji dawa na ufuatiliaji kwa kutumia mfumo wa alama za vidole kutolewa kwa wananchi hasa wenye maambukizi ya VVU.
“Kwa sasa kama taifa tunawasjili wagonjwa kupitia alama za vidole na ni mwezi wa sita sasa tunaendelea kuwasajili na tupo asilimia 98 kama wilaya,wagonjwa wote wanotumia dawa za VVU kwa sasa wamesajiliwa na ni kwa Taifa zima ambapo taarifa zitakuwa zinapatuikana eneo lolote atakalo fika mgonjwa kupata huduma”alisema Minja
Daktari Minja ameeleza kuwa katika viashiria wanavyo pimwa navyo vya 95-3 hali ya kujitambua,kutumia dawa na waliopo kwenye dawa za kufubaza virusi vya UKIMWI ni mkubwa .
“Viashiria tunavyopimwa navyo vya 95-3 ni kwamba asilimia 95 wenye maambukizi ua UIKIMWI kutambua halli zao ni asilimia 98,95 ya pili ni walio na maambukizi kuanza kutumia dawa ni asilimai 99.1 na 95 ya mwisho kwa walipo kwenye dawa wawe wamefubaza virusi vya UKIMWI kwa zaidi ya asilimia 95 wao wamefikia asilimia 97.1 hivyo asilimia 96 YA wenye maambukizi ya VVU katika wilaya hiyo wanajitambua na asilimia 99.1 wanatumia dawa” alifafanua Dk.Minja.
Amesema kuwa baada ya zoezi hilo kuanza baadhi ya watu walikuwa na hofu ya kujisajili kupitia mfumo wa vidole na baada ya elimu kutolewa wananchi wameelewa na kujisajili.
Awali Diwani wa Kata ya Masama Kusini Cedrick Pangani ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya UKIMWI ya Wilaya ameshauri elimu itolewe kwa wananchi huku akieleza umuhimu wa zoezi hilo.
“Serikali imeanzisha zoezi hili mahususi ili kusiwe na mwingiliano kuwa mtu akichukua dawa sehemu nyingine taarifa ionekane kote,hakuna udhalilishaji katika hili ,wapo waliokuwa wanajiandikisha wilaya ya Hai na kwenda kuchukulia dawa Simanjiro ila kwa sasa ukijiandikisha eneo moja na kutoa elimu kwa wananchi” Pangani