Latest Posts

WIZARA YA MAJI KUWAKUTANISHA WADAU WA USALAMA WA MABWAWA MWANZA

 

Wizara ya Maji imeandaa mafunzo ya usalama wa mabwawa Ili kuhakikisha maji ya mabwawa yanaendelea kuwa Salama kwa Matumizi.

Kauli hiyo imetolewaa na Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Robet Sunday ambaye amemwakilisha Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Mwajuma Waziri katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa mikutano Wizara ya Maji Mtumba jijini Dodoma.

Mafunzo hayo yanafanyika Jijini Mwanza kuanzia Oktoba 21 hadi 23 mwaka huu yakilenga kuendelea kutoa elimu kwa wadau na wataalamu wa mabwawa ili kuhakikisha ujenzi na uendelezaji wa mabwawa ya maji na mabwawa ya tope sumu Ili kulinda mazingira na vyanzo vya maji.

Aidha mafunzo hayo yameandaliwa na Wizara ya Maji kwa kushirikiana na taasisi ya chemba ya migodi Tanzania na Kampuni ya City Engineering.

Washiriki wengine katika mafunzo hayo ni wamiliki wa mabwawa makubwa ya Maji, wataalamu wa mabwawa waliosajiliwa, na wataalamu kutoka serikalini ambao wanahusika na usimamizi wa mabwawa ya Maji na tope sumu.

Mafunzo hayo ya mwaka huu yanabebwa na kauli mbiu ya “usalama wa miundombinu ya mabwawa kuanzia kwenye hatua ya usanifu, utumiaji hadi ufungaji.

Ametumia fursa hiyo kuwaalika watunga sera, wataalamu na wamiliki wa mabwawa ya maji na tope sumu, taasisi na watu binafsi wanaojishughulisha na mabwawa pamoja na wadau wote kujisajili kwenye mafunzo ya usalama wa miundombinu ya mabwawa, kuanzia hatua ya usanifu, utumiaji hadi ufungaji, kupitia tovuti ya https://damsafetyconference.tz

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!