Latest Posts

WIZARA YA MAJI NA BENKI YA MAENDELEO UJERUMANI (KfW) KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI

Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso, akiwa jijini Frankfurt, Ujerumani tarehe 9 Oktoba 2024, ametembelea makao makuu ya Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) na kukutana na viongozi wa benki hiyo kwa lengo la kuimarisha na kukuza ushirikiano kati ya Serikali ya Shirikisho la Ujerumani na Tanzania katika uwekezaji kwenye sekta ya maji.

Waziri Aweso ameeleza shukrani zake kwa ushirikiano uliopo kati ya pande hizi mbili katika utekelezaji wa miradi ya maji nchini Tanzania, akiahidi kuendeleza na kudumisha ushirikiano huo, huku KfW wakiahidi kuendelea kushirikiana na Tanzania na kuwezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya miradi hiyo.

Akitoa maelezo zaidi, Waziri Aweso amezungumzia miradi mikubwa inayoendelea, ikiwemo Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi mkoani Simiyu wenye thamani ya shilingi bilioni 400. Mradi huu utaboresha upatikanaji wa maji katika wilaya za Bariadi, Busega, Itilima, Meatu na Maswa. Viongozi wa KfW walipongeza juhudi za utekelezaji wa mradi huo.

Miradi mingine iliyojadiliwa ni pamoja na Mradi wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Babati, na miradi ya uboreshaji wa usafi wa mazingira katika miji ya Lindi, Kigoma, na Sumbawanga. Pia, mpango wa ujenzi wa mradi wa maji Tunduma-Vwawa-Mlowo ulikuwa sehemu ya mazungumzo.

Kupitia ushirikiano huu, Wizara inatarajia kupata Euro milioni 15 kwa ajili ya miradi ya maji mkoani Lindi na Mtwara, sambamba na manufaa mengine.

KfW walimpongeza Waziri Aweso kwa kufanikisha Hati Fungani ya Mamlaka ya Maji Tanga (Tanga Green Bond) na kuahidi kushiriki katika kufanikisha hati fungani kwa mamlaka za maji nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!