Latest Posts

ZAIDI YA NYUMBA 432 ZAEZULIWA NA MVUA ULANGA

 

Zaidi ya nyumba 432 zimebomoka na nyingine kuezuliwa paa baada ya mvua iliyoambatana na upepo kunyesha katika kata ya Iragua Wilaya ya Ulanga na kuathiri vijiji vinne vilivyopo kwenye kata hiyo.

Wakizungumza na JAMBO TV wananchi hao wameiomba serikali kuingilia kati kutatua changamoto hiyo kwani hadi sasa hawana makazi ya kudumu kutokana na adha hiyo.

Mvua hiyo imesababisha madhara kwenye makazi ya wananchi, taasisi za umma ikiwemo ofisi ya kijiji,baadhi ya madarasa ya shule ya msingi Iragua hali inayokwamisha utolewaji wa huduma muhimu kwa wananchi.

Kilio hicho kikamfikia mbunge wa jimbo la Ulanga Salim Alaudin Hasham na kutoa ahadi za kuwapatia huduma muhimu ikiwemo mfuko mmoja wa unga kwa kila kaya iliyoathiriwa na mvua hizo na kuiomba serikali kutoa msaada wa haraka ili kunusuru madhara yanayoweza kutokea

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!