Latest Posts

ZITTO KUISHITAKI SERIKALI KWA ‘KUWAHAMISHA KWA NGUVU’ WATU WA USINGE, TABORA WATOKE MAENEO YAO

Kutokana na madhila yaliyowapata wakazi wa kijiji cha Usinge wilaya ya Kaliua mkoani Tabora, baada ya serikali ‘kuwahamisha kwa nguvu’ katika eneo lao lililogeuzwa kuwa hifadhi, Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe ameamua kuishtaki serikali ya Tanzania kwa Tume ya Haki za Binadamu.

Zitto ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wananchi wakati wa mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika jimbo la Kaliua mkoani humo, Agosti 7, 2024.

“Tumekuwa na migogoro ya ardhi Kigoma Kusini, watu wamechukua ardhi mwekezaji anasema kwamba hii ni ardhi yangu serikali imejenga miundombinu ya umwagiliaji, tumekutana na hali hiyo Kilato, serikali imeingilia sehemu ya ardhi ya wananchi, tumekutana mambo hayo Mbarali, Ngorongoro kule mmesikia Wamasai wanahamishwa, tuna tatizo kubwa sana katika suala zima la ardhi” Ameeleza Zitto.

Amesema kuwa migogoro hiyo ya ardhi katika maeneo mbalimbali ya nchi yamesababisha ongezeko la uhasama baina ya wananchi na wananchi, serikali na wananchi na serikali na wawekezaji, na wakati mwingine imesababisha kupotezwa kama maisha ya raia.

“Watu wanapoteza maisha kwa sababu serikali na taasisi zake zinataka mipaka zaidi, kuna vijiji 947 Tanzania leo tunavyozungumza vimeathiriwa na mipaka ambayo serikali inaongeza dhidi ya wananchi wake, la pili migogoro ya wawekezaji dhidi ya raia, tumetoka huko Katavi kuna sehemu tumekwenda Ruhambwe tumekuta serikali imewapa wawekezaji ardhi ya wananchi wote halafu inawahamisha wale wananchi bila kujua inawapeleka wapi, kwa hiyo wananchi wamekasirika Kaya 800 zimeachana na CCM wamejiunga na ACT Wazalendo ili angalau wapate chombo cha kuwasemea” Ameeleza Zitto.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!