Latest Posts

USHIRIKIANO WA ADEM NA PEACE CORPS KUBORESHA MAFUNZO YA WALIMU WA SAYANSI NA HISABATI NCHINI TANZANIA

 

  • Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) Dkt. Maulid J. Maulid pamoja na wataalamu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na OR-TAMISEMI leo tarehe 24 Oktoba, 2024 ameshiriki katika hafla ya kupokea taarifa ya mafunzo yaliyoendeshwa na ADEM kwa kushirikiana na Peacecorps kwa wataalamu kutoka nchini Marekani ambao huja nchini kujitolea kufundisha masomo ya Sayansi na Hisabati katika Shule za Sekondari nchini. Mafunzo hayo yamefanyika kwa kipindi cha wiki 10 katika Chuo cha Ualimu Korogwe.

Baada ya kuendeshwa kwa mafunzo hayo, programu ya Peacecorps imewaalika Walimu Wakuu na Walimu Wakuu Wasaidizi ambao watapokea wataalamu hao wa kujitolea katika Shule zao ili kuwajengea uwezo wa namna ya kushirikiana nao na kufanya nao kazi wakati watakapokuwa wakifundisha katika Shule wanazozisimamia.

Wakuu wa shule na Wakuu wa Shule wasaidizi wapatao 30 walioshiriki zoezi hilo la kupokea maelekezo wametoka katika Mikoa ya Dodoma, Njombe, Iringa, Kilimanjaro na wengine wametoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Wataalamu hao kutoka nchini Marekani watafanya kazi nchini katika kipindi cha Miaka miwili kuanzia Mwezi Januari 2025.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!