Latest Posts

UVCCM MKOA WA GEITA YASEMA  USHINDI WA KISHINDO NI LAZIMA

 

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Geita, Manjale Magambo, amesema chama hicho kina kila sababu ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu ujao kutokana na mafanikio makubwa ya maendeleo yaliyotekelezwa.

Akizungumza na viongozi wa kata za Lwenzera, Lubanga, Nkome, na Nzera wakati wa ziara yake inayohusisha jumla ya kata 122 za mkoa wa Geita, Magambo alisisitiza kuwa miradi mingi ya kimkakati imekamilika, jambo linaloonyesha dira sahihi ya ushindi kwa CCM.

“Tuna kila sababu ya kutembea kifua mbele kwa sababu maendeleo yaliyofanyika ni ushahidi tosha wa dhamira njema ya chama chetu kwa wananchi. Ni wajibu wetu kuhakikisha tunashinda kwa kishindo,” alisema Magambo.

Ziara hiyo inalenga kuhamasisha wanachama wa CCM na vijana wa UVCCM kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu ili kuhakikisha chama kinapata ushindi mkubwa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!