Latest Posts

51 WALIOKATIWA MAJI WAREJESHEWA HUDUMA BILA FAINI MUSOMA

Katika kuadhimisha wiki ya Maji Jumla ya wakazi 51 waliokuwa wamesitishiwa huduma ya Maji na mamlaka ya Maji safi na usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA)katika Manispaa ya Musoma Mkoani mara wamerejeshewa huduma hiyo bila faini.

Akizungumza kaimu Meneja wa mamlaka hiyo Edward Range amesema urejeshwaji wa huduma hiyo nikufatia ofa iliyotolewa na Rais DKT Samia Suluhu Hassan ikiwa nijitihada ya kuwaboreshea huduma wananchi na kuwajali.

Range Alisema pamoja na jitihada hizo za serikali bado kunachangamoto kubwa ya wananchi kutokulipa bili kwa wakati pamoja na fedha za makusanyo kutokidhi matumizi ikiwemo matengenezo.

Baadhi ya Wenyeviti wameipongeza Serikali huku wakiiomba mamlaka hiyo kuangalia namna ya kuondoa changamoto ya mambomba kupasuka

Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amewonya wale wote wanaoishiriki kwa namna moja ama nyingine kuharibu miundombinu hiyo watachikulia hatua za kisheria.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!