Latest Posts

DC KATWALE: ULAWITI NA UBAKAJI NI MWIKO NDANI YA MANISPAA YA TABORA

 

Mkuu wa wilaya ya Tabora, Deusdedith Katwale amefanya ya kikazi na ukaguzi wa miradi mbalimbali katika kata za Tumbi, Malolo, na Chemchem yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 1.8.

Baada ya ukaguzi huo, aliendesha mikutano mitatu na wananchi ambapo alisikiliza kero zao na kuzitatua ambapo pia wananchi wengi walipata ufumbuzi wa kero zao.

Kuhusu miradi ya maendeleo, Mheshimiwa Katwale alitoa maelekezo kadhaa, akisisitiza kuwa hatarajii kusikia kuwa kuna mradi ambao haujakamilika kwa sababu ya upungufu wa fedha.

 

Aliagiza kuwa fedha zinazotolewa na serikali ni lazima zitumike kikamilifu na kutosha katika kutekeleza miradi hiyo kwa ubora uliokusudiwa.

Aidha, aliagiza watendaji wa serikali kwa kushirikiana na wananchi kupambana na wimbi la wahamiaji haramu.

Pia, Mheshimiwa Katwale aliwataka wananchi kuongeza juhudi katika kulinda mila na desturi za Kitanzania, hasa kwa kukemea vitendo vya ushoga na ulawiti ambavyo kwa sasa vimekuwa tatizo hata mashuleni.

Mheshimiwa Katwale aliwaasa wananchi kuachana na vitendo vya ukatili, mauaji, ukatili wa kijinsia, ubakaji, na ulawiti, akisema kuwa vitendo hivyo ni vya kusikitisha na kutisha. Aliongeza kuwa wahusika wa matendo hayo ni watu tunaowafahamu, majirani zetu, na ndugu zetu. Aliwaomba wananchi kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa kutoa taarifa pindi wanapoona viashiria vya ukatili.

Alisisitiza kuwa Wilaya ya Tabora haitapenda kusikia matukio kama haya yakijirudia na akahimiza ushirikiano wa jamii katika kuzuia matukio hayo.

Vilevile, alionya juu ya taarifa za vitendo vinavyohatarisha amani ya nchi vinavyotengenezwa na watu wasio na nia njema, ambao wanajaribu kuchonganisha wananchi na serikali yao.

 

Kufuatia hilo, amdwataka wananchi kuwa waangalifu na watu hao na kuhakikisha hawawapi nafasi ya kuvuruga amani ya nchi na imani kwa serikali.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!