Hoteli ya kitalii Tulia Retreat and Spa, iliyopo mkoani Arusha, imeendelea kuwa moja ya hoteli zinazovutia watalii wa kimataifa kwa zaidi ya miaka 10. Hoteli hii, iliyoko mitaa ya kifahari jijini Arusha, imeboresha mazingira yake na inaendelea kutoa huduma za kipekee kwa wageni wa aina mbalimbali.
Mkurugenzi wa Tulia Group of Hotels &Spa Fatima Samantar, ameeleza kuwa hoteli hiyo imekuwa kielelezo cha ubora na mafanikio katika sekta ya utalii.
Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa maboresho ya hoteli hiyo Desemba 9, 2024, Fatima ambaye pia anajulikana kama miongoni mwa Malkia wa Nguvu barani Afrika alisema:
“Hotel yetu hii ya Tulia ni kama mama kwa sababu imezalisha hoteli nyingine hapa Arusha, mtaa wa Sakina, inayojulikana kama Tulia Boutique.”

Fatima aliongeza kuwa maboresho yaliyofanyika Tulia Retreat and Spa yanahakikisha hoteli hiyo inabaki kuwa chaguo la kwanza kwa wageni kutoka mataifa mbalimbali.
Afisa Mkuu wa Mikakati wa Tulia Retreat and Spa, Jasmine Samantar alieleza kuwa hoteli hiyo imechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha uzoefu bora kwa watalii.
“Kwa muda wote, Tulia Group zimekuwa chachu ya watalii wengi kufurahia huduma zinazotolewa hapa. Tunaendelea kuimarisha juhudi zetu ili kulingana na matarajio ya wateja wetu,” alisema Jasmine Samantar

Hafla ya uzinduzi wa maboresho ya Tulia Retreat and Spa ilifanyika Desemba 9, 2024, katika viwanja vya hoteli hiyo. Wageni waliopata nafasi ya kuhudhuria walipata kushuhudia huduma na mandhari mpya ambayo hoteli hiyo imeboresha kwa ajili ya wageni wake.
Kwa miaka 10, Tulia Retreat and Spa imeendelea kuwa alama ya ubora wa huduma za kitalii nchini Tanzania, na maboresho haya ni ishara ya kujituma zaidi katika sekta ya utalii.
