Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Adam Malima, Septemba 7, 2026, amemfariji Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kufuatia msiba wa mumewe, Maalim Hafidh Ameir Hassan, aliyefariki dunia Septemba 7, 2026, Zanzibar.
Malima alifika nyumbani kwa Rais Samia, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, kwa ajili ya kutoa pole na kushiriki katika kipindi hiki cha majonzi kufuatia msiba huo.
Pia RC Malima ametoa pole kwa Rais Samia pamoja na familia, ndugu na jamaa wa marehemu, akiwataka kuwa na moyo wa subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.
