Latest Posts

SAMIA CUP 2025 KUANZA KUTIMUA VUMBI KWA KISHINDO KIGAMBONI, TIMU 32 KUSHIRIKI

Mdhamini Mkuu wa mashindano ya Samia Cup 2025, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Togabe Super Sembe, Doto Samweli Rweikiza (mwenye kanzu ya bluu) akikabidhi vifaa vya michezo kw timu shiriki za mashindano hayo leo Jumamosi Februari Mosi, 2025

Afisa Habari na Matukio wa Taasisi ya Twende Pamoja na Mama Sports Promotion Omari Kombe (katikati), akielezea mwenendo wa namna ya Mashindano ya Samia Cup 2025 yatakavyotekelezwa katika wilaya ya Kigamboni. Kulia kwake ni Mwenyekiti wa mashindano hayo Rashid Mfaume Suleiman 
Mdhamini Mkuu wa mashindano ya Samia Cup ambaye pia ni Mkurugenzi wa Togabe Super Sembe, Doto Samweli Rweikiza akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari kuelekea kuanza kwa mashindano hayo leo Jumamosi Februari Mosi, 2025 Makunduchi Vila Hotel, Kigamboni jijini Dar es Salaam
Wawakilishi wa timu 32 zitakzoshiriki Mashindano ya Samia Cup 2025 wakiwa katika hafla ya kukabidhiwa vifaa vya michezo maalum kwa ajili kuwawezesha kushiriki mashindano hayo

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni na Afisa Utamaduni wa Halmashauri hiyo, Lunzegere Kilala akitoa salamu za serikali kuelekea mashindano hayo

 

Mashindano ya mpira wa miguu ya Samia Cup 2025 yanayolenga kuibua vipaji na kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita, yanatarajiwa kuanza rasmi Februari 07, 2025, katika viwanja vya Mji Mwema, Kigamboni.

Katika hafla ya ugawaji wa vifaa kwa timu shiriki iliyofanyika leo Jumamosi Februari Mosi, 2025, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni ambaye pia ni Afisa Utamaduni wa Manispaa hiyo, Lunzegere Kilala, amewahimiza wachezaji kushiriki kwa nidhamu na malengo ya kuinua vipaji vya vijana, huku akisisitiza kuwa michezo ni fursa ya ajira kwa Watanzania.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano, Rashid Mfaume Suleiman, amesema mashindano hayo yameandaliwa na Taasisi ya Twende Pamoja na Mama Sports Promotion ili kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuendeleza michezo nchini.

Timu 32 kutoka Dar es Salaam zinatarajiwa kushiriki, huku mshindi wa kwanza akitarajiwa kuondoka na shilingi milioni 2, wa pili shilingi milioni 1, na wa tatu shilingi 500,000.

Mashindano hayo pia yamedhaminiwa na Makunduchi Vila Hotel, Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), na Jamii Dispensary, huku ulinzi na usalama ukiimarishwa kwa ajili ya ustawi wa mashindano hayo.

Singa Peter Muga ambaye ni mwakilishi wa timu ya Mapepe FC kutoka Ubungo, amesisitiza kuwa, wamekuja Kigamboni kuonesha vipaji vyao na kushindana kwa kiwango cha juu.

Mashindano hayo yanaungwa mkono kwa karibu na Manispaa ya Kigamboni, ikishirikiana na Chama cha Soka Wilaya ya Kigamboni (KDFA) kuhakikisha ligi inafanyika kwa kuzingatia taratibu, sheria, na kanuni za mchezo.

Kwa upande wao, mashabiki na wadau wa Michezo wameeleza kuwa, wanatarajia kushuhudia ligi ya kuvutia inayolenga kukuza vipaji vya soka nchini.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!