Latest Posts

KADA WA CCM ATOA ANGALIZO KUELEKEA UCHAGUZI

Na Helena Magabe, Tarime

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jackson Kangoye, amesisitiza umuhimu wa wanachama wa chama hicho kuwa na maadili mema kwa kuepuka kuchafuana wenyewe kwa wenyewe kuelekea uchaguzi, hali ambayo inaweza kusababisha ugumu wa kuuza wagombea wao kwa wapiga kura.

Amesema ni utovu wa nidhamu kutumia lugha chafu kuwachafua watia nia pamoja na viongozi waliopo madarakani. Ameonya kuwa iwapo kuna watu wanaowatumia kufanya hivyo, wanapaswa kuonywa. Aidha, amekumbusha kuwa hivi karibuni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Emmanuel Nchimbi, alizungumzia suala hilo.

“Hata Dk. Nchimbi, Katibu Mkuu wa chama, alilizungumzia hilo juzi juzi. Leo sisi wana-CCM tunatukanana ndani kwa ndani, tunachafuana vya kutosha, halafu tunatakiwa kutoka nje na kutafuta mgombea mmoja wa kumuunga mkono. Tutapata wakati mgumu kumuuza,” amesema Kangoye.

Kangoye, ambaye aliwania kuteuliwa nafasi ya aubunge wa Jimbo la Tarime Mjini mwaka 2020 kupitia uchaguzi ndani ya chama hicho, amesema anaamini kwamba, kama ilivyo kwa kipaji, mtu anaweza kuwa kiongozi wa kuzaliwa, lakini pia kiongozi anaweza kutengenezwa na kuandaliwa ili awe bora, mradi tu akubali kujifunza kadri anavyoelekezwa.

Kwa upande mwingine, amesema mfumo wa uchaguzi wa wagombea uliopo kwa sasa ni mzuri kwani unampa fursa mgombea kuwa chaguo la wengi na si matakwa ya wachache. Ameeleza kuwa kwa sasa wapiga kura wanaanzia hadi ngazi ya shina, tofauti na miaka ya nyuma ambapo kundi dogo la watu lilikuwa na uwezo wa kumilikiwa na mtu mwenye pesa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!