
Inatajwa kuwa kwa sasa Taifa linakabiliwa na maradhi yasiyoambukiza, hali ambayo inahusishwa na vifo vinavyotokana na ajali za barabarani,katika mwaka 2024, kati ya ajali 1,735 zilizotokea ajali 1,715 ziligharimu maisha ya watu.
Hayo yamebainishwa mkoani Morogoro na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri Aridhini , Augustus Fungo, katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Mtumiaji wa Huduma Mbalimbali za Maji,Nishati Usafiri wa ardhini na anga pamoja na mawasiliano Duniani ambapo amesisitiza kuwa ni wakati sasa kwa wabunifu wa barabara kubuni miundombinu itakayomlinda mtumiaji wa barabara.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Watumiaji wa Huduma, Daudi Daudi amesema kuwa leo asasi za kiraia zimekutanishwa kwa ajili ya kutoa hamasa na elimu kwa jamii kuhusu haki ya mtumiaji huduma,Nao baadhi ya washiriki wameeleza umuhimu wa mabaraza hayo katika kuhakikisha haki za watumiaji zinaheshimiwa.