Latest Posts

MVAMBA: WANANCHI WA IRINGA VIJIJINI WAMETAMBUA UTENDAJI WA RAIS SAMIA

Mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Iringa Vijijini, Anold Mvamba, amesema wananchi wa wilaya hiyo hawana deni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutokana na kazi kubwa aliyoifanya katika kuwaletea maendeleo yanayoonekana.

Akizungumza wakati wa kikao kazi cha mafunzo kwa makatibu wa siasa na wenezi kutoka kata 28 za Iringa Vijijini, Mvamba alisema uongozi wa Rais Samia umejidhihirisha kwa kusimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya kijamii inayogusa maisha ya watu wa kawaida.

“Kutoka ujenzi barabara, vituo vya afya, maboresho kwenye sekta ya elimu, miundombinu na pembejeo kwa wakulima pamoja na upatikanaji wa maji safi, yote haya ni mafanikio yanayodhihirisha uongozi wa mfano wa Rais wetu, wananchi wanaliona hili, na kwa hakika, hawana deni naye,” alisema Mvamba.

Mvamba aliongeza kuwa kwa kutambua mchango mkubwa wa Rais Samia katika maendeleo ya taifa, kilichobaki kwa wananchi wa Iringa Vijijini ni kumthibitisha kwa kura ya ndiyo katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Aidha, alisisitiza umuhimu wa viongozi wa chama katika ngazi zote kuendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya sita, sambamba na kujenga mshikamano na amani katika jamii.

Kikao hicho kililenga kuwajengea uwezo wenezi wa chama katika kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi, ikiwa ni pamoja na kuimarisha uhamasishaji wa siasa safi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!