Latest Posts

KIGAMBONI YAVUA SAMAKI TANI ELFU 18, MAPATO BIL 2.1

Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Dalmia Mikaya amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 jumla ya samaki waliovuliwa na kuuzwa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kigamboni ni tani 18,896.82 na Sekta ya uvuvi imeweza kukusanya mapato jumla ya Tsh 2, 155, 863,128.

DC Dalmia amesema mafanikio hayo pamoja na jitihada nyingine yamechangiwa pia na awamu ya kwanza ya mkopo wa boti zinazotolewa na Serikali kwa Wavuvi hivyo amewataka wanufaika wa awamu ya pili kutumia vema fursa hiyo ili wavune zaidi ya kiwango hicho cha awamu iliyopita.

DC Dalmia amesema hayo Julai 16,2025 Wilayani Kigamboni wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila kwenye hafla ya kukabidhi boti 13 za uvuvi zenye thamani ya Tsh. bilioni 2 kwa vikundi vya Mikoa ya Pwani na Dar es salaam ambazo zinatarajiwa kuwanufaisha zaidi ya Wavuvi 205 wa Mikoa hiyo, boti hizo zimekabidhiwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Ashatu Kijaji.

Waziri Dkt. Kijaji amesema kuwa ugawaji wa boti hizo ni sehemu ya mkakati wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan uliolenga kuboresha sekta ya Uvuvi nchini ambapo wanufaika wanajumuisha makundi manne ambavyo ni watu binafsi, makampuni na vikundi vya Wavuvi.

Boti hizo zilizotolewa ni sehemu ya boti 120 zinazotarajiwa kutolewa kwenye awamu ya pili ya Mkopo huo wenye masharti nafuu ambapo mpaka kukamilika kwa awamu zote mbili jumla ya boti 280 zinatarajiwa kukopeshwa kwa Wavuvi nchini

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!