Latest Posts

WANAWAKE CCM KIBITI WATIA FORA KURA ZA MAONI, WAJUMBE 1,661 WASHIRIKI KUPIGA KURA

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani, Tatu Mkumba, ameongoza Mkutano Mkuu wa jumuiya hiyo na kuratibu zoezi la upigaji kura za maoni kwa ajili ya kupata wagombea wa nafasi za udiwani viti maalum, kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Zoezi hilo limefanyika katika viwanja vya CCM wilayani humo ambapo jumla ya wajumbe 1,661 walishiriki kupiga kura, likiwa ni sehemu ya mchakato wa ndani wa chama kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Akifungua mkutano huo, Tatu Mkumba aliwataka wajumbe hao kufanya uchaguzi wa haki na kuzingatia maslahi ya wanawake wa Wilaya ya Kibiti, akisisitiza kuwa waliochaguliwa wanapaswa kuwa chachu ya maendeleo ya wanawake na jamii kwa ujumla. Kikao hicho kiliratibiwa na Katibu wa UWT Kibiti, Rabia Selemani.

Kwa mujibu wa Msimamizi wa uchaguzi wa kura za maoni, Zainabu Mketo, jumla ya wagombea 19 waligombea katika tarafa tatu za Kibiti, Mbwela na Kikale. Haya hapa ni matokeo ya walioongoza katika kila tarafa:

Tarafa ya Mbwela:

  • Swaumu Mwangi – kura 923
  • Mwajuma Dagwa – kura 906
  • Ashura Ngonwe – kura 684

Tarafa ya Kikale:

  • Mwashabani Mlawa – kura 1,265
  • Amina Mapande – kura 351

Tarafa ya Kibiti:

  • Latifa Augustino – kura 1,338
  • Mwamtimu Hamza – kura 962
  • Salha Mjanja – kura 874

Upigaji kura huo ulienda kwa amani na utulivu huku wajumbe wakijitokeza kwa wingi, hali inayoonesha mshikamano na nidhamu ndani ya jumuiya hiyo

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!