Latest Posts

WAHAMIAJI 60 WAFARIKI DUNIA BAADA YA BOTI KUZAMA BAHARINI

Zaidi ya wahamiaji 60 wamepoteza maisha baada ya boti waliokuwa wakisafiria kuzama katika pwani ya Yemen, kufuatia hali mbaya ya hewa siku ya Jumapili, tukio ambalo limeelezwa na mashirika ya kimataifa kuwa ni la kusikitisha na kutisha.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) nchini Yemen, ajali hiyo imetokea katika jimbo la Abyan kusini mwa Yemen. Miili 68 tayari imepatikana, huku watu 12 wakinusurika na makumi wengine bado hawajulikani walipo.

“Boti hiyo ilikuwa imebeba takriban watu 157, wengi wao wakiwa ni raia wa Ethiopia waliokuwa wakijaribu kuvuka kuelekea mataifa ya Ghuba kwa matumaini ya maisha bora,” amesema Abdusattor Esoev, Mkuu wa IOM Yemen.

Yemen imeendelea kuwa njia hatari lakini ya kawaida kwa wahamiaji kutoka Pembe ya Afrika, hasa kutoka Ethiopia na Somalia, wanaolenga kuvuka hadi Saudi Arabia na nchi jirani za Kiarabu kutafuta ajira.

IOM imesema kuwa tukio hili linaongeza idadi ya wahamiaji waliopotea au kufariki katika safari za hatari kwa bahari katika miezi ya hivi karibuni, huku wito ukitolewa kwa mataifa ya kikanda na mashirika ya kimataifa kuongeza jitihada za kulinda maisha ya wahamiaji na kukabiliana na usafirishaji haramu wa binadamu.

 

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!